Kupitia Shangazi Power tunalenga kubadilisha simulizi za kijamii, kitamaduni na kihistoria kuhusu wanawake katika nafasi zao za raia wanaojitambua kama njia ya kuhamasisha ushiriki wao katika demokrasia.

Tafiti nyingi zimeonyesha kuwa mifumo ya ukandamizaji, kama vile udikteta, na mfumo dume mara nyingi huingiliana na kuimarishana. Hili limedhihirika barani Afrika ambapo mfumo dume umeendelea kukita mizizi katika ngazi zote za jamii, na heshima kwa Kiongozi Mwenye Nguvu (The Strong Man Syndrome) bado unakubalika na kuvumiliwa. Katika miaka ya hivi karibuni tumeona kuimarika kwa hali hii Afrika Mashariki na kusababisha kuongezeka kwa ukandamizaji na upinzani dhidi ya wale wanaopinga viongozi au mfumo dume, Mifumo dhalimu Afrika Mashariki imekuwa na changamoto tangu uhuru (na hata wakati wa kupigania uhuru) wanawake ambao walikabiliwa na changamoto mbili za kushinda mfumo wa kisiasa na kukaidi mfumo dume ndani ya harakati na jamii kwa ujumla.

Uchunguzi umeonyesha kuwa zaidi ya vuguvugu maalum la jinsia, na mara kwa mara bila kutambuliwa, wanaharakati wanawake wameshiriki na kuongoza harakati nyingi za haki na uhuru kote ulimwenguni. Hata hivyo, wanaharakati wanawake wanaendelea kukabiliwa na changamoto nyingi - wanaitwa walegevu, mseja, wabaya wa sura, na wasiotakiwa. Hili ni jaribio la kutaka kuwavua utu wao na hivyo kudhoofisha uanaharakati wao. Mara nyingi shughuli zao hazizingatiwi na mitandao ya kawaida ya kijamii, hii pia hutokana na mifumo dume iliyokita mizizi. Tunatambua umuhimu wa kuangazia na kukuza majukumu na mafanikio ya wanaharakati wanawake waliojitolea, ili kupanua nafasi yao, kuongeza mitandao yao, na kuhimiza wanawake zaidi kujihusisha na uanaharakati.

Nguvu ya Shangazi* - Shangazi Power:


* Kuna msemo wa Kiswahili usemao: "Shangazi ni Baba" ambao unaashiria kuwa kama Baba hayupo, Shangazi (dada yake baba) huwa na kauli ya mwisho kama mtoa maamuzi. Neno hili ni la heshima sana na ni tofauti na neno linalotumiwa kwa ujumla la "auntie". Ilipata heshima na hadhi ya pekee nchini Tanzania wakati wa utawala wa Rais John Magufuli, ambapo mwaka 2018 alitishia watu kutoka. Kusini mwa Tanzania na kuwaonya katika hotuba yake wasijaribu kuandamana vinginevyo atatuma vyombo vya dola kuwapiga "mashangazi" wao. Hotuba hii ilijaa unyanyasaji wa vitisho dhidi ya wanawake kiasi kwamba iliwakasirisha baadhi ya wanawake ambao hadi wakati huo, walikuwa mstari wa mbele kuikosoa vikali utawala wa Magufuli. "Shangazi" mashuhuri ni pamoja na Fatma Karume, Maria Sarungi, Vicensia Shule. Na baada ya muda, zaidi na zaidi walijiunga na safu hii. Leo Shangazi inabakia kuwa ya heshima, njia ya kutambua wanawake ambao wana msimamo wanapinga ubabe, wanapigania haki na kusimama imara dhidi ya mfumo dume.

Video Zinazohusiana na Mradi:

Bibi Titi Mohammed
Wangari Maathai
Jerotich Seii
Stella Nyanzi
Fatma Karume
Wanjeri Nderu
Judy Muthoni
Evelyn Acham
Ananilea Nkya
Sarah Bireete