Karibu MwanzoDotOrg,

Maono yetu ni kuwawezesha watu wa Afrika, kwa kutumia teknolojia ili kukuza sauti zao. Ni dhamira yetu kuwahudumia watu wa Afrika Mashariki kwa maudhui yanayoakisi tofauti za maoni na utamaduni wao, kutajirisha akili zao na kupanua mitazamo yao, na hivyo kuwasaidia kuboresha maisha yao na kuimarisha jamii zao.

Sisi ni asasi ya kiraia inayojihusisha na uzalishaji wa maudhui yenye maslahi kwa umma, na inayozingatia Maendeleo, Haki za Binadamu, Uhuru wa Kujieleza, Uhuru wa Vyombo vya Habari, na Usawa wa Kijamii. Tunaamini kuwa jukumu moja muhimu ni kusaidia kuziba mianya kushughulikia katika vyombo vya habari na mapengo ya mawasiliano ndani ya asasi ya kiraia na hivyo kutoa suluhusho zinazohitajika, kuandaa maudhui na mafunzo kwa watendaji na mashirika ya kiraia.

Tunatilia maanani sana shughuli za Jumuiya ya Afrika Mashariki na raia wa nchi wanachama: Kenya, Uganda, Tanzania, Burundi, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Sudan Kusini. Pia tunaelekeza nguvu zetu katika nchi zinazozungumza Kiswahili nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, na kwa mataifa ambayo yana uhusiano wa kihistoria na Jumuiya kama vile Somalia, Sudan na Ethiopia.

Maudhui yetu yanapakiwa na kusambazwa kupitia Mwanzo TV na Mwanzo TV Plus huko YouTube na kupitia majukwaa yetu mengine ya mitandao ya kijamii.

Miradi ya Sasa:

Shangazi Power